UNYAMA..! MAMA AMUUA MWANAE WA MIEZI 3 KWA KUMPIGA MPINI WA JEMBE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/unyama-mama-amuua-mwanae-wa-miezi-3-kwa.html
MWANAMKE
mmoja, Habiba Swedi (21), mkazi wa Kijiji cha Tagamenda, Mkoa wa
Iringa, amemuua mtoto wake wa miezi mitatu, Christina Kalolo kwa kumpiga
mpini wa jembe.
Pia, mwanamke huyo alimjeruhi mtoto wake wa miaka saba, Grace Kalolo kwa kumpiga na mpini huo.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana asubuhi nyumbani kwa mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Baba mzazi wa watoto hao, Bosco Kalolo, aliiambia MTANZANIA, kwamba mke wake alifanya unyama huo baada ya kurukwa na akili.
“Tuliamka
asubuhi vizuri tu, lakini baada ya muda mfupi, mke wangu ni kama
alichanganyikiwa kwa sababu alichukua mpini wa jembe na kutaka kunipiga
nao.
“Nilijizuia
ili asinipige, na wakati wa purukushani nilifanikiwa kukimbia. Alipoona
ameshindwa kunidhuru, aliingia ndani na kuwageukia watoto waliokuwa
wamelala kitandani.
“Nilipokuwa nje, nilisikia akipiga vitu kwa nguvu, kumbe alikuwa akiwapiga watoto kwani walianza kulia kwa sauti.
“Nilipochungulia
ndani, nilimuona akiwapiga watoto kwa kutumia mpini, yaani niliumia
sana kwa sababu nilijua kama nikimfuata anaweza pia akaniumiza.
“Nilipoona
hali hiyo, nilikimbia kwa majirani kuomba msaada, na walipofika
tulimkuta huyo mdogo ameshafariki dunia kwa sababu alikuwa
amepondwapondwa kichwa,” alisema Kalolo.
Kalolo
alisema yeye na majirani walishirikiana kumdhibiti mwanamke huyo kwa
kumtoa nje, kisha wakaanza kuwahudumia watoto wengine wawili waliokuwa
wamejeruhiwa.
“Tulipofanikiwa
kumtoa nje, tulirudi ndani kwa ajili ya kuwapatia msaada watoto wengine
kwa sababu mmoja kati yao alikuwa na hali mbaya kwa sababu alikuwa
ameumizwa kichwani,” alisema.
Kwa mujibu wa Kalolo, ameishi na mkewe kwa miaka 10 na kufanikiwa kupata watoto wane, akiwamo Christina aliyefariki.
SOURCE. MTANZANIA
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA